Simba yapania kuendeleza ubabe dhidi ya Coastal Union leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1 Feb 2020
Simba yapania kuendeleza ubabe dhidi ya Coastal Union leo

Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba leo wanashuka uwanja wa Taifa kuikaribisha Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom

Baada ya kuibuka na ushindi kwenye michezo yote minne iliyopita, Simba watakuwa na nafasi ya kuzidi kujikita kileleni kwani mpaka sasa wamejikusanyia alama 44, alama nane zaidi ya Azam Fc inyowafuata nafasi ya pili

Kuelekea mchezo huo ambao utapigwa saa kumi jioni, kocha Mkuu wa mabingwa hao wa nchi Sven Vandenbroeck anatarajiwa kufanya mabadiliko ya kikosi chake kilichocheza mchezo dhidi ya Namungo Fc

Sven amesema mchezo uliopita hawakucheza vizuri kwa kuwa baadhi ya wachezaji wake walikuwa wamechoka huku akibainisha kuwa wapo ambao hawawezi kucheza mechi nyingi mfululizo

Mabadiliko makubwa pengine yanaweza kuonekana kwenye safu ya ulinzi ambayo kwa siku za karibuni imeingia lawamani kutokana na kuruhusu mabao mfululizo

SImba itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mabao 8-1 kwenye mchezo wa mwisho ambao ulizikutanisha timu hizo uwanja wa uhuru msimu uliopita

 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’