Vinara wa ligi kuu ya Vodacom, Simba wameyaaga mashindano ya kombe la Mapinduzi baada ya kuchapwa bao 1-0 na URA ya Uganda.
Simba ilihitaji kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo ili iweze kutinga nusu fainali.
Bao la Kalama Deboss alilofunga kwenye dakika za majeruhi za kipindi cha kwanza limeiwezesha URA kutinga nusu fainali ikiwa kinara wa kundi B baada ya kufikisha alama 10.
Simba ilitengeneza nafasi kadhaa za kufunga lakini kukosekana kwa umakini kwa safu ya ushambuliaji kwa mara nyingine kumeigharimu Simba.
Hicho ni kipigo cha pili mfululizo katika michuano hiyo baada ya juzi kulazwa bao 1-0 na Azam FC.
Aidha katika hali ya kushangaza wachezaji Shiza Kichuya, Jonas Mkude na Nocolas Gyan waligoma kukaa kwenye benchi baada ya kutolewa na Kaimu Kocha Mkuu Masudi Djuma.
Simba sasa inarejea jijini Dar es salaam kujiandaa na mcihezo ya ligi kuu ya Vodacom itakayoendelea baada ya kukamilika kwa michuano hiyo ya kombe la Mapinduzi

ADVERTISE HERE