Wachezaji Yanga wapewa motisha

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Sep 2017
Wachezaji Yanga wapewa motisha
Ili kuhakikisha Yanga inafanya vizuri viongozi wa Yanga wameanzisha utaratibu wa kuwapa motisha wachezaji kila wanaposhinda au kutoka sare nje ya jiji la Dar es salaam.

Afisa habari msaidizi wa Yanga, Godlisten Anderson 'Chicharito'ameliambia gazeti la Mwanaspoti kuwa utaratibu huo umeanzishwa ili kuwapa changamoto wachezaji kuhakikisha wanapata matokeo kwenye kila mchezo.

"Ni hivi, kila mechi itatoka pesa, kama wachezaji wakipata ushindi kila mmoja anapata laki moja, timu ikipata sare ugenini hupata nusu ya posho ya ushindi lakini wakitoa sare Dar es Salaam hawapewi kitu," amefunguka Chicharito.

Yanga inashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi ikiwa imeshuka dimbani mara nne. Imeshinda michezo miwili na kutoka sare michezo miwili pia.

Kwa mahesabu hayo wachezaji wamejikusanyia jumla ya Tsh 250,000/-. Sare ya 1-1 dhidi ya Lipuli haikuwapa bonas kwa kuwa ilipigwa kwenye dimba la nyumbani.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’