Kiungo James Kotei amebainisha waziwazi mapenzi yake kwa klabu ya Simba baada ya kugoma kujiunga na Yanga iliyokuwa ikimtaka kwa mkopo
Kotei aliyejiunga na Kaizer Chiefs mwezi Juni 2019, aligomea dili hiyo ya kutua Yanga huku akisisitiza kuwa timu pekee inayoweza kumrudisha Tanzania ni klabu ya Simba
Katika mahojiano maalum na blog hii, Kotei amesema kwa sasa wakala wake anashughulikia taratibu za kuvunja mkataba na klabu ya Kaizer Chiefs
Amesema anaweza kurejea kwao Ghana kuungana na familia yake lakini kama Simba itahitaji kumrejesha nchini yuko tayari
"Ninaipenda Simba, nawaheshimu mashabiki wake kwani walinipa upendo mkubwa wakati nipo Tanzania. Nisingeweza kujiunga na Yanga kwani ni kama nafanya usaliti," amesema Kotei
Hii ni nafasi kwa uongozi wa Simba kumrejesha nchini mwamba huyo kwani mwenyewe ameonyesha utayari wa kurejea Msimbazi