Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema ukiondoa nadharia ya kuwa kwenye mchezo wa dabi jambo lolote linaweza kutokea, lakini anaamini kikosi cha Simba kina nafasi kubwa zaidi ya kushinda mchezo dhidi ya Yanga keshokutwa
Akihojiwa na redio moja maarufu mapema leo, Manara amesema mpira ni mchezo wa wazi, kwa jinsi vikosi vya timu zote vilivyo, ni mwendawazimu pekee ambaye anaweza kusema Yanga inaweza kuifunga Simba wakati huu
"Namfahamu vizuri Mkwasa, ameshiriki michezo ya dabi akiwa mchezaji na kocha. Najua siku hiyo atakuja na mfumo wa kupaki basi kwani hiyo ndio njia pekee ambayo itawanusuru na kapu la mabao," ametamba Manara
"Lakini akithubutu kufunguka, nakuhakikishia tutawafunga zaidi ya mabao matano"
Simba itakuwa mwenyeji wa mchezo huo utakaopigwa uwanja wa Taifa kuanzia saa 11 jioni