Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amefanya mabadiliko ya kikosi kinachoikabili Ndanda Fc kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Nahodha John Bocco ambaye amekuwa nje kwa zaidi ya miezi mitatu, leo amepata nafasi ya kuanza huku Meddie Kagere akianzia benchi
Aidha kiungo Said Khamis Ndemla nae amepata nafasi ya kuanza leo dimba la kati sambamba na Jonas Mkude
Kennedy Juma nae ameanza safu ya ulinzi wa kati sambamba na Erasto Nyoni ambaye amerejea kikosini hivi karibuni baada ya kupona majeraha
Kikosi kilichoanza:
1. Aishi Manula
2. Haruna Shamte
3. Gadiel Michael
4. Kennedy Juma
5. Erasto Nyoni
6. Jonas Mkude
7. Ibrahim Ajib
8. Said Ndemla
9. John Bocco
10. Sharaff Shiboub
11. Francis Kahata
Sub
Beno Kakolanya
Shomari Kapombe
Tairone Da Silva
Clatous Chama
Mzamiru Yassin
Deo Kanda
Meddie Kagere