Mwandila ajenga pumzi, stamina ya wachezaji Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Jul 2019
Mwandila ajenga pumzi, stamina ya wachezaji Yanga

Katika  kuhakikisha kikosi cha Yanga kinakuwa imara zaidi msimu ujao, Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Noel Mwandila amewaanzisha tizi la kibabe wachezaji hao kwa kuanza na mazoezi ya kujenga stamina ili kuweza kuwa imara.

Kikosi cha Yanga kipo mkoani Morogoro ambako kimeweka kambi kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 23.

Yanga imeweka kambi Morogoro bila ya kocha Mkuu Mwinyi Zahera ambaye yupo nyumbani kwake nchini Ufaransa baada ya kutolewa katika michuano ya Afcon ambapo anatarajia kuwasili mkoani Morogoro Julai 17

Mratibu wa Yanga Hafidh Saleh amesema kuwa, Kocha Mwandila ameanza na mazoezi ya stamina ya kukijenga kikosi kabla ya kuanza mazoezi magumu ili kuhakikisha anawaweka
wachezaji sawa.

"Mazoezi anayoyatoa kocha kwa sasa ni yale ya stamina ya kujenga wachezaji kama inavyojulikana mazoezi ya mwanzoni mwa msimu, wachezaji wanafanya mazoezi asubuhi na jioni huku mwalimu akiwa anaendelea kukipanga kikosi ili kiweze kuwa imara," amesema

"Baada ya kumaliza mazoezi hayo, ndio kocha atakapoendelea na mazoezi mengine kwa ajili ya kukiimarisha kikosi ambapo mwalimu akifika ataendelea pale atakapopakuta"

GPL

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
8h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
17h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
23h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’