Januari 04 tutawapigia 'One Touch' - Manara

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
29 Dec 2019
Januari 04 tutawapigia 'One Touch' - Manara

Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amekuja na 'slogan' ya 'One Touch' kuelekea mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Yanga

Mchezo huo utapigwa Januari 04 2020 kwenye uwanja wa Taifa

Tayari shamrashamra kuelekea mchezo huo zinashika kasi

Manara amesema hana wasiwasi na kikosi cha Simba kwani anajua siku hiyo utapigwa mpira mwingi

"Siku hiyo utapigwa mpira mwingi sana halafu mipasi kuliko yote..! Game hii slogan yetu ni ONE TOUCH," ametamba Manara

Simba itakuwa mwenyeji wa mchezo huo na kwa mwenendo wanaokwenda nao chini ya kocha mpya Sven Vandenbroeck, matumaini ni makubwa kwa Wanamsimbazi, siku hiyo kalamu ya mabao inaweza kushuhudiwa

Simba inajivunia rekodi ya kupata ushindi mnono zaidi dhidi ya watani zao Yanga miaka ya hivi karibuni

Ilikuwa mwaka 2012 mabingwa hao wa nchi walipoibuka na ushindi wa mabao 5-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa

Wengi wanatamani kuona rekodi hiyo au ile ya mwaka 1976 ya ushindi wa mabao 6-0 ikirudiwa Januari 04 2020

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
11m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
3h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
21h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’