Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba leo jioni kinashuka kwenye uwanja wa Uhuru kumenyana na Lipuli Fc ukiwa ni mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Mabingwa hao wa nchi wanashuka dimbani kunogesha sikukuu ya Krismasi ambayo Wanasimba watakuwa miongoni mwa wanaosherehekea
Hii itakuwa nafasi nyingine kwa Simba kuzidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi kama wataweza kuibuka na ushindi
Aidha mchezo huo utakuwa wa kwanza (kwenye ligi) kwa benchi jipya la ufundi linaloongozwa na Sven Vandenbroeck akisaidiana na Selemani Matola
Mchezo utaanza saa kumi kamili Alasiri
Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amesema timu ilikamilisha maandalizi yake salama jana na wako tayari kuwapa furaha mashabiki wao leo
ADVERTISE HERE