Kipigo cha Azam Fc chafanya mchezo dhidi ya Simba kuwa mgumu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
6 Jan 2018
Kipigo cha Azam Fc chafanya mchezo dhidi ya Simba kuwa mgumu
Mabingwa watetezi wa kombe la Mapinduzi Azam FC watakuwa kwenye mtihani mgumu kuhakikisha wanashinda mechi yao ya Kundi A ili kufuzu kucheza nusu fainali ya michuano hiyo inayoendelea visiwani Zanzibar, Azam wamepoteza mchezo wao wa tatu dhidi ya URA kwa kufungwa goli 1-0.

Azam ipo katika nafasi ya pili hadi sasa kwenye Kundi A ikiwa na pointi sita nyuma ya URA ambayo ina pointi saba baada ya kucheza mechi tatu.

Endapo Azam itapoteza mchezo wake dhidi ya Simba, moja kwa moja itajikuta nje ya mashindano hayo kwa sababu Simba itafikisha pointi saba huku ikiwa na mechi moja mkononi wakati Azam watakuwa wamemaliza mechi zao za hatua ya makundi.

Azam imeshacheza mechi tatu hadi sasa, imeshinda mechi mbili (Mwenge 1-2 Azam, Jamhuri 0-4 Azam ) huku wakipoteza mchezo mmoja (Azam 0 -1 URA).

Kundi A lina timu tano URA (Uganda), Simba, Azam (Tanzania bara), Jamhuri na Mwenge (Zanzibar).

Mechi ya Azam vs Simba itachezwa leo Jumamosi January 6 kuanzia saa mbili na robo usiku.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
6h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
12h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
15h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’