Cannavaro awatoa hofu mashabiki

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Sep 2017
Cannavaro awatoa hofu mashabiki
Nahodha wa Yanga Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema wachezaji wamerejea kwenye majukumu yao baada ya kumalizana na uongozi kuhusu madai yao.

Yanga imeendelea na mazoezi leo kwenye uwanja wa Uhuru ikiwa ni siku ya pili baada ya kutokea sintofahamu miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa wakidai mishahara ya miezi kadhaa.

Akizungumza kwa ufupi baada ya mazoezi leo asubuhi, Cannavaro amesema uongozi umewahakikishia kukamilisha madai yao kabla ya mchezo wa Jumamosi dhidi ya Ndanda na hivyo kuondoa hofu iliyokuwepo.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Idara ya Fedha ya Yanga, Baraka Deusdedit, amesema kuchelewa kwa mishahara ya wachezaji kumesababishwa na bajeti ndogo wanayopewa na wadhamini kulinganisha na mahitaji ya klabu.

Amesema klabu imebuni vyanzo mbalimbali vya mapato ili kukabiliana na hali hiyo.

Pia kumekuwa na taarifa kwamba huenda aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji akarejea kwenye nafasi yake ili aweze kusaidiana na uongozi kufanya mageuzi ya kiuendeshaji.

Kabla hajakumbwa na matatizo Manji aliwasilisha kusudio la kutaka kuikodisha Yanga (kutumia nembo na jina) kwa miaka 10 ambapo tayari alishaunda kampuni ya Yanga Yetu ambayo ingesimamia klabu.

Mpango huo ungeiwezesha Yanga kupata asilimia 25 ya mapato katika kipindi chote cha mkataba.

Kampuni hiyo ingelipa mishahara ya wachezaji pamoja na maslahi yao ya kila siku kuhakikisha Yanga inafanya vizuri.

Kampuni hiyo pia ingesimamia ujenzi wa Uwanja wa kisasa wa Yanga huko Kigamboni (Eneo limeshataifishwa na Serikali) pamoja na vyanzo vingine vya mapato ambavyo vingekuwa mali ya Yanga baada ya muda wa mkataba kumalizika.

Hata hivyo mpango huo ulipingwa vikali na baadhi ya wadau wa Yanga akiwemo Katibu wa Baraza la Wazee, Mzee Akilimali.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’