Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao kwenye mchezo wa kombe la FA raundi ya tatu dhidi ya Arusha Fc
Mchezo huo utapigwa kesho Jumapili kwenye uwanja wa Uhuru kuanzia saa kumi Alasiri
Manara amesema wachezaji wanahitaji sapoti ya mashabiki ili kuhakikisha wanashinda mchezo huo
Aidha, Manara 'amechombeza' kuwa mchezo huo ni mgumu kuliko mchezo wa ligi January 04 2020 ambao ni dhidi ya Yanga
"Njooni Wanasimba kesho mtusapoti timu yenu,tupo Uhuru stadium kuwakabili Arusha FC kwenye kombe la Shirikisho la Azam, ni saa Kumi Alasiri," amesema
"Tutambue game ya kesho ni ngumu kuliko ile ya tarehe nne ambayo kwetu ni sawa na Dr na kumchoma sindano mgonjwa wake,,ni chaguo la tabibu tu,amchome ngapi na kwa muda gani"
"Tuje kwa wingi uwanja wa Uhuru"
Mchezo huo utakuwa wa kwanza kwa benchi jipya la ufundi linaloongozwa na kocha mkuu Sven Vanderbroeck anayesaidiwa na Selemani Matola
Mashabiki wa Simba watakuwa na nafasi ya kushuhudia mbinu za kocha huyo kwa mara ya kwanza