Mshambuliaji mpya wa Yanga, Juma Balinya, kwa mikwara, hajambo hasa baada ya kusema anawasili nchini na vifaa vyake vyote muhimu vya kufanyia mazoezi kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Juma aliyesajiliwa na Yanga akitokea Klabu ya Polisi ya Uganda, alisema hahitaji kusubiri vifaa ya mazoezi kutoka kwa benchi la ufundi la timu hiyo, chini ya Kocha Mwinyi Zahera, kwani amejinunulia vya kwake.
Mshambuliaji huyo, aliyetarajiwa kuwasili nchini jana, alisema amepanga kuja na vifaa vya aina mbalimbali vya kufanyia mazoezi binafsi, wakati atakapokuwa nje ya program ya kocha wake.
Mganda huyo, alisema wachezaji wengi wanashindwa kuonyesha kiwango kutokana na kutegemea kila kitu kutoka kwa benchi la ufundi au uongozi wa klabu yao.
“Nimejiwekea mfumo wa kuwa na vifaa vyangu vya mazoezi na huwa navitumia kama niko mapumziko ili kuendelea kujiweka fiti,” Balinya amenukuliwa na gazeti la Bingwa
Alisema mipango yake kwa sasa ni kuhakikisha anaisadia timu hiyo katika harakati ya kutwaa ubingwa wa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.