Wachezaji Simba wabanwa, watoro kambini kukiona

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Dec 2019
Wachezaji Simba wabanwa, watoro kambini kukiona

Kocha Mkuu wa mabingwa wa soka nchini Sven Vandenbroeck amewataka wachezaji wote kukaa kambini hata kama hawapo katika programu zake huku akiwataka viongozi kutotoa ruhusa zisizo na maana kwa wachezaji wake

Vanderbroeck ametaka masuala yote yanayohusu wachezaji wake yapitie kwake

“Kocha ametaka wachezaji wasipewe ruhusa kabla ya yeye kupewa taarifa na kuridhia kulingana na tatizo la mchezaji"

“Lakini pia wachezaji wote hivi sasa watakuwa kambini hata kama hawapo kwenye programu za kocha ili kupunguza nafasi ya wao kufanya mambo yanayowaathiri mchezoni na ameweka wazi hayupo tayari kumvumilia mvivu katika mazoezi,” kilisema chanzo cha habari.

Simba inaendelea na mazoezi katika uwanja wa Mo Simba Arena kikijiandaa na michezo ya mashindano ya Azam Federation Cup dhidi ya Arusha United mwishoni mwa wiki hii.

Mbali na mechi hizo lakini pia Wekundu wa Msimbazi wanakabiliwa na michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Lipuli, KMC, Ndanda FC kisha watakutana na Yanga Januari 4, mwaka huu.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
6h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
6h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
9h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’