Yanga kuanza kujifua Morogoro

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Jul 2019
Yanga kuanza kujifua Morogoro

Kikosi cha Yanga kitaanza maandalizi yake ya msimu mpya mkoani Morogoro baada ya kocha Mwinyi Zahera kupendekeza timu iweke kambi mkoani humo

Awali kulikuwa na taarifa kuwa Yanga ingeweka kambi nje ya nchi

Aidha, Yanga itaanza maandalizi bila ya Zahera ambaye anakabiliwa na majukumu ya timu ya Taifa huko Misri

DR Congo ilifuzu hatua ya 16 bora michuano ya Afcon 2019 ambapo Jumapili Julai 07 itacheza na Madagascar

Yanga imeanza maandalizi mapema kutokana na timu hiyo kuwa na wachezaji wapya wengi ambao watahitaji muda kuweza kuzoeana

Pia Julai 27 itahitimisha tukio la wiki ya Mwananchi litakalofanyika uwanja wa Taifa kwa kucheza mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya moja ya timu kutoka nje ya nchi

Kampeni ya michuano ya ligi ya mabingwa nayo itaanza mapema katika kipindi cha wiki nne zijazo

Zahera awasilisha program za mazoezi

Katika hatua nyingine kocha Mwinyi Zahera atayari amewasilisha program ya mazoezi ambayo itasimamiwa na kocha Msaidizi Noel Mwandila

Mcongoman huyo anaweza kuchelewa kujiunga na kambi ya Yanga kutegemea na hatma ya DR Congo kwenye michuano ya Afcon

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’