Sven ataka muda zaidi kuisoma Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
15 Dec 2019
Sven ataka muda zaidi kuisoma Simba

Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba, Sven Ludwig Vandenbroeck, licha ya kuomba siku 10 ili kukaa kwanza na timu hiyo kabla ya kuzungumza rasmi na vyombo vya habari nchini, amegusia kitu ambacho ni wazi atakuwa ameugusa 'mshipa wa fahamu' wa uongozi, wanachama na mashabiki wa
timu hiyo.

Baada ya kumtambulisha Jumatano usiku, uongozi wa klabu hiyo ulitangaza kuwa juzi kocha huyo angezungumza na waandishi wa habari, lakini baada ya wanahabari kuwasili eneo la tukio wakatangaziwa kuwa mkutano huo umeahirishwa na kwamba Sven ameomba apewe siku 10 za kukaa na wachezaji wake kabla ya kuzungumza na vyombo vya habari.

"Naomba nipewe muda kama wa siku kumi ndio nitaweza kuweka hadharani mikakati yangu kwa sababu bado sijakaa muda mrefu na timu, nikikaa nao ndio nitajua nini cha kuzungumza," alisema.

Hata hivyo, kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa klabu hiyo, kocha huyo alifunguka kwa kugusia jambo ambalo ni kama ameushika mshipa wa fahamu wa uongozi, wanachama na mashabiki wa timu hiyo baada ya kueleza sehemu ya mikakati yake ambayo ndiyo kiu kubwa ya klabu hiyo.

“Lengo la kwanza ni kushinda ubingwa wa Ligi Kuu. Nataka kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika, nataka kucheza mashindano ya CAF. Nataka Simba iwe kwenye hatua kubwa na kupata matokeo mazuri.

"Kilichonivutia Simba cha kwanza ni wingi wa mashabiki. Ni jambo la kufurahisha kuona mashabiki 60,000 wakikushangilia inakupa hisia za kipekee,” Sven alisema.

Sven jana aliendelea kukinoa kikosi hicho katika mazoezi yanayoendea kwenye Uwanja wao wa Simba Mo Arena, Bunju jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Mwina Kaduguda alisema:

"Kikao kilikuwa kifanywe leo [juzi] kocha azungumze na waandishi wa habari, lakini tumeahirisha tutakifanyika siku nyingine itakayopangwa," alisema Kaduguda.

GPL

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
19h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’