Ametoka fundi mmoja Ajib, wameingia mafundi wengi

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
30 Jun 2019
Ametoka fundi mmoja Ajib, wameingia mafundi wengi

Mkataba wa nahodha wa Yanga Ibrahim Ajib unafikia tamati leo na pengine kesho atatangazwa kwa mbwembwe zote huko Msimbazi ambako inaelezwa amesaini mkataba wa miaka miwili

Hata hivyo kwa usajili uliofanywa na mabingwa hao wa kihistoria, ni dhahiri Ajib kinara wa pasi za mabao msimu uliomalizika hataacha pengo Jangwani

Kwenye safu ya kiungo Yanga imeongeza watu wanne matata Abdulaziz Makame, Mapinduzi Balama, Patrick Sibomana na Issa Bigirimana ambao wanatarajiwa kuibadili kabisa Yanga

Huku ikisajili washambuliaji matata Juma Balinya, Maybin Kalengo na Sadney Urikhob

Msimu uliopita Yanga ilimtegemea zaidi Ajib katika kutengeneza mabao ambapo timu hiyo ilitumia mipira ya krosi na adhabu kufunga idadi kubwa ya mabao yake

Ajib aliifungia Yanga mabao sita na kutoa pasi 15 za mabao ambapo Mcongomani Heritier Makambo ndiye aliyenufaika zaidi ya krosi za Ajib akifunga mabao matano kati ya 17 aliyoweka kambani

Uongozi wa Yanga umempa baraka zote Ajib kwenda kusaka maisha sehemu nyingine ukitambua mchango wake kwenye kikosi cha timu hiyo msimu uliopita

Katika mkutano na waandishi wa habari wiki iliyopita, Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela alisema timu hiyo ilifanya mazungumzo na Ajib lakini hawakufikia muafaka hivyo kumpa uhuru wa kuamua kuhusu muktakabali wake

Yanga imeongeza nyota wapya 13 kwenye kikosi chake cha msimu ujao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’