Usajili dirisha dogo kusubiri kocha mpya Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
6 Dec 2019
Usajili dirisha dogo kusubiri kocha mpya Simba

Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa amesema wanakusudia kufanya maboresho ya kikosi kwenye dirisha dogo litakalofunguliwa ndani ya kipindi cha siku 10 zijazo

Hata hivyo hilo litakuwa jukumu la kocha mpya akayetua kurithi mikoba ya Patrick Aussems

Kumekuwa na tetesi kuwa Simba inamuwania mshambuliaji Tuisila Kisinda anayekipiga AS Vita Club

Mazingisa amesema mapendekezo ya usajili yatatolewa na kocha mpya hivyo kwa sasa wameweka nguvu zao kwenye mchakato wa kumpata kocha huyo

"Masuala ya usajili kwa sasa hatushughuliki nayo, bado tunahitaji kupata kocha mkuu ambaye atakifanyia tathmini kikosi kisha kutoa mapendekezo yake," amesema

Hata hivyo inaelezwa kabla Aussems hajatimuliwa alikuwa tayari amewasilisha ripoti ya mapendekezo yake kwa ajili ya maboresho wakati wa dirisha dogo

Aussems alipendekeza kusajiliwa mshambuliaji mmoja atakayesaidiana na washambuliaji waliopo

 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
15h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
20h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
23h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’