Kilimanjaro Stars, Zanzibar Heroes uso kwa uso Jumapili

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3 Dec 2019
Kilimanjaro Stars, Zanzibar Heroes uso kwa uso Jumapili

Tanzania Bara itafungua dimba na ndugu zao, Zanzibar Jumapili kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge inayotaraiwa kuanza Desemba 7 hadi 19 mjini Kampala nchini Uganda.

Baada ya kufungua dimba na Zanzibar Heroes, Kilimanjaro Stars, mabingwa wa 1975, 1994 na 2010 watarejea uwanjani Desemba 10 kumenyana na Kenya kabla ya kukamilisha mechi za Kundi C kwa kumenyana na Djibouti Desemba 12.

Zanzibar wao baada ya kupambana na Tanzania Bara Jumapili, watarejea uwanjani Desemba 10 kumenyana na Djibouti kabla ya kukamilisha mechi za kundi lao kwa kukipiga na Kenya Desemba 12.

Kundi A linaundwa na wenyeji, Uganda, Burundi, Ethiopia na Eritrea, wakati Kundi B linaundwa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Sudan, Sudan Kusini na Somalia.

Timu mbili za juu kutoka kila kundi zitaingia Robo Fainali zikiungana na mbili nyingine zitakazomaliza na wastani mzuri katika nafasi ya tatu.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
38m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
12h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
18h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’