Wito rasmi kwa wadau kukarabati jengo la Yanga Jangwani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Jun 2019
Wito rasmi kwa wadau kukarabati jengo la Yanga Jangwani

Taarifa kwa vyombo vya Habari

Uongozi wa klabu ya Yanga umetoa wito rasmi kwa wadau na wapenzi wa klabu ya hiyo ambao wangependa kufanya ukarabati wa vyumba katika Jengo la Makao makuu ya klabu hiyo lililopo mitaa ya Twiga na Jangwani jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Yanga, Dkt. Mshondo Msolla, amesema Kamati ya utendaji iliyoketi mwishoni mwa wiki imebariki kuanza kwa zoezi hilo kupitia wadau wenye mapenzi mema na klabu hiyo, ili kuwawezesha wachezaji kuishi katika jengi hilo.

"Kwenye halfa ya Kubwa Kuliko nililieleza hili, nashukuru Kamati ya Utendaji imelipitisha, sasa rasmi tunawaalika wadau, ikiwa ni mwananchama mmoja, Tawi la Yanga, Kundi la WhatsApp au hata kampuni kufika klabuni kuanzia Alhamisi, ambapo tutakuwa tumeanisha gharama za ukarabati wa kila chumba hivyo watachagua kulingana na uwezo wao, " alisema Dkt. Msolla.

Amesema kukatabatiwa kwa vyumba katika Jengo la Yanga, kutasaidia kuondoa gharama kubwa ambazo timu hiyo imekuwa ikizitumia kwenye hoteli wakati wa kambi za mazoezi ya kawaida hasa timu inapokuwa jijini Dar es Salaam.

"Tutatoa nafasi kwa vyumba kupewa majina ya wadau waliofanya ukarabati, mfano kama ni tawi la Makao Makuu, basi Chumba kitaitwa Makao Makuu kama watapenda, hivyo hii ni nafasi nyingine wa wadau wetu kusaidia maendeleo ya klabu yao kwa kuiepusha na gharama zinazoweza kuepukika," alisema.

Alisema uongozi umekuwa na maono ya kurejesha uhai wa kila kitu klabuni hapo kama ilivyokua zamani, na hivyo haitakuwa busara kutumia tena pesa zilizochangwa kwa ajili ya ukatarabati huo kwani hiyo haikuwa sehemu ya lengo ya fedha hizo.

Jengo la Yanga lina jumla ya vyumba 28 pamoja na meneo mengine muhimu ikiwamo eneo la kufanyia mazoezi ya Ndani (gym) ambayo pia inahitaji ukarabati mkubwa pamoja na kuwekwa vifaa vya kisasa.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
7h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’