Zimbwe Jr amuaga Aussems

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1 Dec 2019
Zimbwe Jr amuaga Aussems

Nahodha Msaidizi wa Simba Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr', amemuaga aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Patrick Aussems aliyefutwa kazi jana

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, Zimbwe Jr amekuwa mchezaji wa kwanza wa Simba kumuaga kocha huyo aliyeisaidia Simba kutetea ubingwa wa ligi kuu msimu uliopita pamoja na kufika robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

"Tunakushukuru kwa kila kitu, tunakutakia kila la kheri huko uendako," aliandika Zimbwe Jr

Nyota wengine waliotumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kumuaga Aussems ni Clatous Chama na Jonas Mkude ambao wanatajwa kuwa wachezaji na rafiki zake zaidi

Inaelezwa kutimuliwa kwa Aussems kumewashtua baadhi ya wachezaji kwani hawakutarajia kama uamuzi huo ungefikiwa

Tukio hilo pia limeibua sintofahamu miongoni mwa mashabiki lakini ni uamuzi ambao imeelezwa umechukuliwa kwa maslahi mapana ya klabu ya Simba

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
29m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
22h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’