Dirisha la Usajili kwa klabu za Ligi Kuu, Daraja la Kwanza na Daraja la Pili msimu wa 2019/2020 limefunguliwa rasmi.
Dirisha hilo limefunguliwa Juni 15,2019 na litafungwa Julai 31,2019 kwa kutumia mfumo mpya wa usajili(TFF FIFA CONNECT)
Aidha klabu zitakazoshiriki michuano ya CAF msimu ujao ambazo ni Yanga, Simba, Azam Fc na KMC zimetakiwa kukamilisha usajili kabla ya Juni 30 2019 kwa kuwa usajili wa CAF utafungwa rasmi Julai mosi 2019
Baada ya Dirisha kufungwa kutakuwa na wiki moja ya pingamizi ikifuatiwa na Kamati ya Katiba,Sheria na Hadhi za Wachezaji kukaa kupitisha usajili.
ADVERTISE HERE