Baada ya kuifungia Simba mabao mawili jana na kuisaidia kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting, Miraji Athumani amesema atajitahidi kufunga mabao kila anapopewa nafasi ili kuisaidia timu yake lakini pia kujiweka sawa katika mbio za kuwania ufungaji bora wa ligi kuu msimu huu
Miraji amefikisha mabao sita akiwa nyuma ya kinara wa ufungaji mshambuliaji mwenzake wa Simba Meddie Kagere mwenye mabao nane
Mshambuliaji huyo aliyesajiliwa na Simba akitokea Lipuli Fc, amesema anaamini kama kocha ataendelea kumpanga nafasi ya ushambuliaji wa kati ataendelea kufunga
"Zamani nilikuwa nacheza winga lakini sasa kocha ananipanga zaidi kwenye nafasi ya ushambuliaji wa kati. Naamini akiendelea kunipanga nafasi hii nitafunga mabao zaidi," amesema
"Nafahamu haitakuwa rahisi kwani Simba ina washambuliaji mahiri kama Kagere, Bocco na wengineo"
"Nitahakikisha kila ninapopewa nafasi nafunga mabao kama nilivyofanya leo"