Magori apendekeza usajili wa msimu ujao ufanyike mapema

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
26 Oct 2019
Magori apendekeza usajili wa msimu ujao ufanyike mapema

Aliyekuwa Mtendaji wa Simba Crescentius Magori ambaye sasa ni mshauri binafsi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mo, amependekeza Simba kukamilisha michakato yake ya usajili wakati wa usajili wa dirisha dogo

Magori ametoa maoni hayo yakiwa na lengo la kwendana na mabadiliko ya kalenda ya CAF hasa kwa michuano ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho

Msimu huu Simba ilitolewa hatua ya awali michuano ya ligi ya mabingwa, sababu kubwa iliyotajwa kuiponza Simba ni mabadiliko hayo kwani ilianza michuano huku ikiwa haijacheza mechi hata moja ya ligi

UD Songo iliyoitoa Simba, ilikuwa tayari imecheza mechi saba za ligi kuu Msumbiji

Magori amesema Simba iliongeza nyota wengi wapya lakini hawakuwa na muda wa kutosha kuingia kwenye mfumo wa Mwalimu kabla ya michuano hiyo kuanza

Amesema kama usajili utafanyika mapema, baada ya ligi kumalizika timu haitakuwa na mabadiliko makubwa kuelekea michuano hiyo mikubwa barani Afrika kwa ngazi ya vilabu

Β 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
4h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’