Zahera apongeza wachezaji Yanga kwa ushindi dhidi ya Mbeya City

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 May 2019
Zahera apongeza wachezaji Yanga kwa ushindi dhidi ya Mbeya City

Licha ya kuwakosa wachezaji saba wanaougua Malaria, kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amewapongeza wachezaji wa timu hiyo kwa kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City

Zahera amesema katika mchezo wa leo alitumia wachezaji wanne kutoka katika kikosi cha U20

"Tulikosa wachezaji wetu saba wanaumwa Malaria, nimetumia vijana wanne wa U20, nafurahi wachezaji wameweza kutupatia matokeo," amesema

"Tulitengeneza nafasi nyingi, tulipaswa kufunga mabao zaidi, nafikiri leo hatukuwa na nidhamu ya mchezo"

Kuhusu maoni yake baada ya Simba kutwaa ubingwa jana, Zahera ameshikilia msimamo wake kuwa hawakustahili kutwaa ubingwa kutokana na upindishwaji mkubwa wa sheria uliofanywa kuwawezesha washinde taji hilo

"Simba waliwapa ubingwa jana, maoni yangu mie nilicheza mpira ambao uko na sheria, ule sio ubingwa," amesema

"Ninapoishi nakaa na watu wa Simba, wananiambia kweli hata kama mpira wetu tunapenda Simba, tunaona kama sio hivyo"

"Tunapata kikombe lakini ukiangalia sheria kabisa mwaka huu hatungepata kikombe"

Wadau mbalimbali wametoa maoni tofauti juu ya ubingwa wa Simba

Wakati wengine wakiamini kuwa Simba ilistahili ubingwa huo, wapo wanaoamini mazingira yaliyotengenezwa na TFF kwa kuiacha timu hiyo isicheze mpaka michezo 12 wakati nyingine zikiendelea na ligi, yameirahisishia timu hiyo kutwaa ubingwa

cut

"Simba walikuwa na michezo 12 ya viporo. Walikuwa wanafahamu matokeo ambayo wanatakiwa wapate ili watwae ubingwa, pengine hali ingekuwa tofauti kama wangecheza sambamba na timu nyingine," amesema Rajabu Issa kutoka Buguruni

"Umeona wapi na ligi gani duniani ambapo timu moja inakuwa na michezo ya viporo 12? kushiriki ligi ya mabingwa haitoshi kuwa sababu ya kurundikiwa michezo mingi kiasi hicho mbona timu walizokuwa wakishindana nazo zilikuwa zikicheza ligi zao?"

"Hawa Simba baada ya kutolewa kombe la FA walipanga mkakati na TFF kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa ligi kuu kupitia ratiba na hujuma kwa Yanga"

"Angalia mchezo dhidi ya KMC ilikuwa wafungwe lakini refa akawatafutia ushindi kwa nguvu halafu baadae TFF wanatangaza kumfungia mwamuzi wakati mpango umeshakamilishwa"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’