Emmanuel Okwi anatajwa kurejea Msimbazi wakati wa usajili wa dirisha dogo utakaofunguliwa Novemba 15 mpaka Disemba 15
Okwi anayeitumikia Ittihad ya Misri, bado hajaweza kuonyesha makali yake kwenye timu hiyo
Mara nyingi Okwi amekuwa hafanikiwa anapocheza klabu tofauti na Simba, pengine ndio sababu inayomfanya awe anarejea Msimbazi kila mara anapoondoka
Inaelezwa mshambuliaji raia wa Brazil Wilker Da Silva anaweza kuwa hatarini kumpisha Mganda huyo kama hataweza kuonyesha makali yake
Wilker bado hajafikia matarajio ya wengi, kocha Patrick Aussems akitaka mshambuliaji huyo apewe muda zaidi
Tangu kuumia kwa Bocco Simba inamtegemea zaidi Meddie Kagere akisaidiwa na Miraji Athumani 'Sheva'
Simba imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya kufunga mabao kila inapowakosa washambuliaji hao
Katika mabao 10 yaliyofungwa na Simba kwenye ligi, Kagere na Sheva wamefunga mabao tisa
Ni dhahiri Simba inahitaji kusajili mshambuliaji mwingine dirisha dogo, haitakuwa ajabu kuona Okwi akirejeshwa Msimbazi kwa mara ya tatu