Beki wa kulia wa Simba Shomari Kapombe hajajiunga na timu ya Taifa ambayo imeingia kambini kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Rwanda
Tangu kupona majeraha yaliyomuweka nje kwa takribani miezi saba, Kapombe hajaweza kuitumikia timu ya Taifa mara ya mwisho alipoitwa aliomba aachwe ili aweze kuimarisha kiwango chake baada ya kuwa nje kwa muda mrefu
Kapombe ni miongoni mwa nyota saba wa Simba walioitwa kikosi cha Stars ambacho pamoja na mchezo huo wa kirafiki, kinakabiliwa na mchezo wa marudiano dhidi ya Sudan kusaka tketi ya michuano ya CHAN
Wachezaji wengine ni Mohammed Hussein, Gadiel Michael, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin na Miraji Athumani
ADVERTISE HERE