Tuyisenge ataka mamilioni Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 May 2019
Tuyisenge ataka mamilioni Yanga

Tetesi za usajili wa mshambuliaji wa Gor Mahia Jacques Tuyisenge zimezidi kushika kasi ambapo vyombo vya habari nchini Kenya vimeripoti taarifa ya wakala wa mshambuliaji huyo Patrick Gakumba kukiri kuwa na mazungumzo na uongozi wa Yanga

Hata hivyo usajili wa mshambuliaji huyo huenda ukaipa changamoto Yanga kutokana na kiwango kikubwa cha mshahara aliotaka alipwe

Gakumba amesema mteja wake yuko tayari kutua Yanga lakini timu hiyo inahitaji kumlipa mshahara ambao ni mara tatu ya ule anaolipwa na Gor Mahia

Mshahara wa Tuyisenge katika klabu ya Gor Mahia ni zaidi ya Tsh Mil tano hivyo atailazimu Yanga imuandalie mshahara wa zaidi ya Tsh Milioni 15 kwa mwezi!

Inaelezwa mshambuliaji huyo pia anawaniwa na AS Vital Club ya DR Congo

Tuyisenge atakuwa mchezaji huru ifikapo Julai mwaka huu ambapo mkataba wake na Gor Mahia utakuwa umemalizika

Mshambuliaji huyo wa Kimataifa wa Rwanda, anataka kuondoka Gor Mahia baada ya timu hiyo kukumbwa na changamoto kubwa ya kiuchumi inayotishia mustakabali wake licha ya msimu huu kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika

Yanga imedhamiria kukiimarisha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao ambapo michakato ya usajili inaendelea 'kimyakimya'

Β 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’