Kichuya aahidi ubingwa Msimbazi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
27 Dec 2017
Kichuya aahidi ubingwa Msimbazi
Ligi Kuu Bara inatarajiwa kuendelea tena wikiendi hii na timu shiriki zinapaswa zijipange kwelikweli kwani winga ghali zaidi nchini, Shiza Kichuya ametamba atakuja kivingine na kutisha zaidi katika ligi hiyo.

Kichuya anayeongoza kwa kuifungia Simba mabao mengi zaidi tangu msimu uliopita (17) alisema; “Simba tuna raha kukaa kileleni na bila shaka mashabiki wetu watakuwa wana furaha mtaani, hilo linawafanya wapinzani wetu, waumize akili namna ya kurejea kwa kishindo,” alisema.

Kichuya alisema hilo litaleta changamoto kwa wachezaji kutaka kuonyesha ufundi wao na ukubwa wa majina yao mbele ya mashabiki wa timu zao, kitu alichokiona kama kinaongeza umakini wa kazi zao.

“Mchezaji mwenye malengo lazima ajipange na kujiuliza alifanya nini wakati ligi inachezwa na sasa anapaswa kuwa na jipya gani la kusaidia kutimiza malengo yao timu.”

“Nataka Simba ichukue ubingwa, hilo linanifanya niendelee kupambana kuhakikisha ndoto inatimia na kuweka rekodi ya kukumbukwa na vizazi vijavyo,” alisema nyota huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE →
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE →
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →