Nahodha msaidizi wa Yanga Thabani Kamusoko ambaye aliumia katika mchezo wa jana Jumapili dhidi ya Njombe Mji, hali yake inaendelea vizuri kulingana na Daktari wa Yanga, Dk Bavu.
Kamusoko alitolewa dakika nne tu tangu kuanza kipindi cha pili baada ya kuumia. Dk Bavu amesema hakupata madhara makubwa hivyo atakuwemo kwenye kikosi cha Yanga kitakachochuana na Majimaji Jumamosi, Septemba 16.
Mchezaji huyo leo asubuhi hakufanya mazoezi na kikosi cha Yanga.
Aidha Dk Bavu amesema majeruhi wengine walioachwa Dar Amissi Tambwe na Benno Kakolanya wanatarajiwa kurejea dimbani wakati wowote baada ya hali zao kuimarika.

ADVERTISE HERE