Licha ya kuwepo taarifa kuwa Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali, Marco Gaguti amepiga marufuku mashabiki wa mkoa huo kuishangilia Simba kwenye mchezo wa leo, Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema mashabiki wana haki ya kushangilia timu yao
Pamoja na kueleza kushangazwa na kauli hiyo, Manara amesema mashabiki hawataogopa kushangilia
"Utaweza kuifunga midomo ya Wanasimba kwa plasta au gundi gani?," ameandika Manara kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram
"Kitu pekee kitakachowanyima fursa ya kuishangilia leo Simba uwanjani ni bunduki tu"
"Tutashangilia na Insha'Allah tutawafunga halafu uje utuweke lock-up kwa cheo chako"
"Sijui baadhi ya viongozi wetu wanakwama wapi? Yaani utuzuie kushangilia timu yetu ndani ya nchi yetu?Haya tunaita madaraka ya kulevya ambayo Rais wa nchi hii hayataki"
Mashabiki wameendelea kuingia kwa wingi uwanja wa Kaitaba tayari kwa mchezo huo

