Wachezaji Yanga wakutana na viongozi, wamaliza mgomo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Apr 2019
Wachezaji Yanga wakutana na viongozi, wamaliza mgomo

Nahodha Msaidizi wa Yanga Juma Abdul amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuwa wamemaliza tofauti iliyojitokeza jana baada ya kukutana na uongozi wa Yanga

Abdul amesema hawakuwa wamegoma kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari bali walihitaji kuonana na viongozi ili kujadili masuala mbalimbali yanayowahusu wachezaji

Amesema hata hivyo jana walishindwa kuonana na viongozi baada ya kutofautiana muda lakini leo wameweza kuonana nao na wamemaliza changamoto iliyokuwepo

"Niwatoe hofu mashabiki wa Yanga kuhusu suala la mgomo. Mimi kama nahodha msaidizi nawaambia hakuna mgomo wowote wa wachezaji isipokuwa baadhi ya wachezaji tuliuhitaji uongozi wa timu yetu kukaa nao," amesema

"Lakini jana tulitofautina muda, viongozi walikuja muda ambao sisi tulikuwa tayari tumeshaondoka. Lakini leo baada ya kumaliza mazoezi tumekaa na viongozi wetu, kama wazazi wetu wametusikiliza na wametuelewa"

"Hivyo tunaendelea na maandalizi ya mchezo dhidi ya Azam Fc"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
17h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
23h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’