Kagera Sugar imewaondoa Simba kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbao Fc
Ushindi huo umeifanya Kagera Sugar ifikishe alama tisa baada ya kushinda michezo yake yote mitatu
Simba, mabingwa watetezi walikuwa wakiongoza ligi kwa tofauti ya mabao ya kufunga
Simba haikushuka dimbani wikiendi hii kutokana na wachezaji wake wengi kuitwa timu ya Taifa kuelekea mchezo dhidi ya Sudan hapo kesho
Mchezo unaofuata ni dhidi ya hao hao Kagera Sugar, Septemba 26 dimba la Kaitaba mkoani Kagera
ADVERTISE HERE