Ndayiragije ataka ushindi mechi dhidi ya Sudan

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
21 Sep 2019
Ndayiragije ataka ushindi mechi dhidi ya Sudan

KaimuKocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Etienne Ndayiragije, amesema mkakati wake wa kwanza ni kupata ushindi mnono nyumbani ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu fainali za Mataifa Afrika  kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN) zitazofanyika mwakani nchini Cameroon.

Stars itakuwa nyumbani kumenyana na Sudan katika mchezo wa kuwania tiketi ya kushiriki fainali hizo kwa mara pili, utakaopigwa kesho Jumapili saa moja jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Stars ambayo bado haijapata ushindi katika muda wa kawaida tangu ilipoanza kunolewa na Ndayiragije, kocha huyo wa Azam Fc amesema amefanyia marekebisho safu yake ya ushambuliaji ili kuhakikisha wanashinda mchezo huo

Amesema timu iko tayari kuelekea mchezo huo

"Kikosi kipo kamili kwa ajili ya mchezo huo, wachezaji wote wako katika hali nzuri. Kikubwa ni kuhakikisha tunapata ushindi mnono nyumbani ili kujipunguzia kazi ugenini," amesema

"Mchezo huu tutaanzia nyumbani, hivyo lazima tutumie vema faida hiyo, tunatakiwa kwenda ugenini tukiwa na mtaji mkubwa wa mabao, tulishindwa kufanya hivyo dhidi ya Kenya, tukajipa mzigo mzito ugenini, lakini safari hii tunataka kuanza vizuri kwa ushindi nyumbani"

Mchezo wa marudiano baina ya timu hizo utapigwa Oktoba 18 nchini Uganda

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
22h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’