Tutapambana tushinde michezo sita iliyobaki - Zahera

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Apr 2019
Tutapambana tushinde michezo sita iliyobaki - Zahera

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema timu yake bado ina nafasi ya kutwaa ubingwa msimu huu lakini inabidi wapate ushindi katika michezo sita iliyobaki

Zahera amesema wanahitaji kushinda michezo yote sita dhidi ya Azam Fc, Ruvu Shooting, Biashara United, Mbeya City, Tanzania Prisons na Azam Fc

"Ligi bado iko wazi hakuna timu ambayo imejihakikishia ubingwa. Kwa upande wetu hatupaswi kufanya makosa zaidi kwenye michezo iliyobaki ili kuwa na nafasi," amesema

Habari njema kwa Yanga ni kuwa ukiondoa mchezo dhidi ya Biashara United ambao utapigwa mkoani Mara, michezo mingine mitano itapigwa uwanja wa Taifa

Yanga itarudi Dar kumalizia michezo yake ya nyumbani iliyobaki baada ya michuano ya AFCON ya vijana kumalizika April 28 2019

April 29 Yanga itaanza kampeni ya kusaka ushindi katika michezo hiyo kwa kuikabili Azam Fc katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Taifa

Yanga ina michezo miwili dhidi ya Azam Fc na pengine mchezo huo wa April 29 utabainisha hatma ya vinara hao wa ligi katika mbio za ubingwa

Baada ya mapumziko ya Pasaka, kikosi cha Yanga kitaendelea na maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Azam FC ambao utapigwa Jumatatu ijayo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
17h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
23h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’