Aveva, Kaburu waanza kujitetea leo, dhamana yao iko wazi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
20 Sep 2019
Aveva, Kaburu waanza kujitetea leo, dhamana yao iko wazi

Jana Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliwapa dhamana aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na aliyekuwa makamu wake, Geofrey Nyange 'Kaburu' baada ya kuondolewa mashitaka ya utakatishaji fedha

Aveva na Kaburu wamekuwa ndani tangu mwaka 2017 walipokamatwa.

Dhamana hiyo ni kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh.Milioni 30, ambapo hatua hiyo inatokana na washitakiwa hao kukutwa na kesi ya kujibu katika mashitaka 7 isipokuwa mawili ya utakatishaji fedha

Hata hivyo washitakiwa hao walishindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo kurudishwa mahabusu ambapo kesi hiyo itaendelea leo Septemba 20, 2019 kwa ajili ya washitakiwa hao kuanza kujitetea akiwemoaliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hanspope

Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam, Thomas Simba alisema baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi 10 wa upande wa mashitaka ambapo amewakuta na kesi ya kujibu washitakiwa hao katika kosa la 1,2,3,4,7,8 na 9 isipokuwa katika shitaka la 6 na 10 ambayo ni ya utakatishaji fedha

Shitaka la kwanza Aveva na Kaburu wanadaiwa kula njama na kutenda kosa la matumizi mabaya ya madaraka

Katika shitaka la pili la Aveva na Kaburu wanadaiwa kutumia vibaya madaraka yao kwa kuandaa fomu ya kuhamisha fedha Dola za Marekani 300,000 kutoka kwenye akaunti ya Simba iliyoko benki ya CRDB Azikiwe kwenda kwenye akaunti binafsi ya Aveva iliyoko benki ya Barclays.

Shtaka la tatu linalowakabili Aveva na Kaburu inadaiwa kwa pamoja walighushi nyaraka iliyokuwa ikionesha Simba inalipa mkopo wa Dola za 300,000 kwa Aveva kitu ambacho sio kweli

Katika shtaka la nne Aveva katika banki ya CRDB anadaiwa kutoa nyaraka ya uongo ikionesha Simba wanalipa mkopo wa Dola za Marekani 300,000

Shtaka la tano, Aveva anadaiwa kuwa katika Benki ya Baclays Mikocheni alijipatia Dola za Marekani 187,817 wakati akijua zimetokana na kughushi

Shitaka la sita, Kaburu anadaiwa kumsaidia Aveva kujipatia Dola za Marekani 187,817 kutoka kwenye akaunti ya Simba wakiwa wanajua fedha hizo zimetokana na zao la kughushi

Shitaka la saba linawakabili Aveva, Kaburu na Hanspoppe ambao wanadaiwa kughushi hati ya malipo ya kibiashara wakionesha kwamba nyasi bandia zilizonunuliwa na Simba zina thamani ya Dola za Marekani 40,577 huku wakijua kwamba siyo kweli.

Katika shitaka la nane, Aveva anadaiwa kuwasilisha hati ya malipo ya kibiashara ya uongo kwa Levison Kasulwa kwa madhumuni ya kuonesha kwamba Simba wamenunua nyasi bandia zenye thamani ya Dola za Marekani 40,577

Shitaka la tisa, Aveva, Kaburu na Hanspope wanadaiwa kuwasilisha nyaraka za uongo kuonesha kuwa Simba imenunua nyasi bandia zenye thamani ya Dola za Marekani 40,577.

Habari Leo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
31m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
22h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’