Wakitaka kunifungia wanifungie ila sitaacha kusema ukweli - Zahera

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Apr 2019
Wakitaka kunifungia wanifungie ila sitaacha kusema ukweli - Zahera

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amemtaka msemaji wa Simba Haji Manara afuatilie mambo yanayomuhusu zaidi kwani hawezi kumzuia kuongea ukweli kwa madudu yanayofanywa na Bodi ya ligi ya TFF

Juzi Manara aliitaka TFF kumchukulia hatua Zahera akidai kuwa amekuwa akilituhumu shirikisho hilo kuihujumu Yanga huku likiibeba Simba

Zahera amesema kama TFF wanaona anakosea basi wanaweza kumfungia lakini yeye anazungumza mambo ya kweli ambayo yanafanyika na hayako mahali pengine popote duniani

"Niwape mfano, Simba itacheza na Tanzania Prisons Mbeya, halafu itabaki mkoani Mbeya kusubiri kucheza na Mbeya City je huu ni uongo?," alihoji Zahera

"Sasa huyu Manara anayesema Zahera anasema sana anawaambia TFF wanifungie. Kama wanaweza wanifungie lakini mimi sitaacha kusema ukweli"

Yanga iliwahi kucheza Tanga na Coastal Union, kisha ikatakiwa kusafiri kwenda Singida kucheza na Singida United halafu siku mbili baadae kurudi tena Tanga kucheza na JKT Tanzania

Ukiangalia ratiba ya michezo ya viporo ya Simba, itacheza michezo yote ya kanda ya ziwa kisha itaelekea Mbeya halafu kurudi jijini Dar es salaam kwani michuano ya AFCON ya vijana itakuwa imemalizika

Aidha ratiba hiyo huenda ikaipa nafasi Simba kucheza michezo yote ya ugenini kwanza halafu kumalizia nyumbani michezo ya kukamilisha ligi kwani imepangiwa kucheza michezo saba mfululizo ugenini

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
13h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’