Unaweza kusema Simba imepabia kwelikweli mchezo dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa wiki ijayo kutokana na mazoezi wanayofanya
Mabingwa hao watetezi wameuchukulia mchezo dhidi ya Kagera Sugar kwa uzito mkubwa pengine ni kutokana na timu hiyo inayonolewa na Meckie Mexime kuanza kujenga mazoea ya kuifunga Simba
Kikosi cha Simba leo asubuhi kiliendelea kujifua kwenye uwanja wa Gymkhana chini ya kocha Patrick Aussems
Aussems ameweka wazi kuwa hayuko tayari kupoteza mchezo dhidi ya Kagera Sugar msimu huu
Katika mazoezi ya leo washambuliaji John Bocco, Meddie Kagere na Deo Kanda wote walikosekana kutokana na majeruhi
Wakati Bocco akiendelea na program matibabu, Kagere na Kanda wana majeraha ya kawaida na watakuwa tayari kuivaa Kagera Sugar wiki ijayo
ADVERTISE HERE