Mexime aanza tambo kuelekea mchezo dhidi ya Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
17 Sep 2019
Mexime aanza tambo kuelekea mchezo dhidi ya Simba

Baada ya kupata ushindi mara mbili mfululizo Ligi Kuu Tanzania Bara, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Mexime, amesema wataendelea kuifunga Simba katika mchezo unaofuata.

Kagera Sugar wanatarajia kukutana na Simba Septemba 26, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, mikoani Kegera.

Msimu uliopita, Kagera Sugar iliifunga Simba michezo yote miwili ambayo ilipata ushindi wa mabao 2-1 katika uwanja wao wa nyumbani na ilishinda bao 1-0 iliporudiana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, Mexime alisema wanaendelea kujipanga na malengo yake ni kuendelea kuifunga Simba, hata kama wataanzisha wachezaji wote wa kigeni.

Alisema pamoja na Simba kuwa na wachezaji wengi wa kigeni ambao wana viwango vizuri uwanjani, lakini hawawezi kupata pointi tatu kutoka kwao.

"Hata kama Kocha wa Simba (Patrick Aussems) ataamua kuwaanzisha wachezaji wake wote wa kigeni haitotusumbua, kwani lazima tuwafunge na rekodi zinajieleza," Mexime aliliambia
Bingwa

"Kile kilichotokea msimu uliopita tuliwafunga nyumbani na ugenini, lazima msimu huu kijirudie, Simba watazionea timu nyingine si Kagera Sugar ikiwa chini yangu"alisema Mexime.

Tayari Kagera Sugar imeshinda mabao 2-0 dhidi ya Biashara United, kisha ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Alliance, wakati Simba ilianza ligi hiyo kwa kuifunga JKT Tanzania mabao 3-1 na baadae ilitoa kipigo cha mabao 2-1 kwa Mtibwa Sugar

Timu zote zina alama sita na tofauti ya mabao matatu ya kufunga na kufungwa

Msimu huu kikosi cha Simba chini ya kocha Patrick Aussems kina kila sababu ya kufuta uteja kwa Kagera Sugar, ambayo sasa kocha wake Mexime amefanya kuwa ni utamaduni wake kuifunga Simba

Katika misimu mitatu iliyopita, Simba imeifunga Kagera Sugar mara mbili tu wakati timu hiyo imeshinda michezo minne

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
8h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
14h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
17h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’