Nahodha wa kikosi cha Yanga Ibrahim Ajib amesema waamuzi wamekuwa wakiwakwamisha kupata matokeo kwenye baadhi ya michezo kutokana na maamuzi yao yasiyo na haki
Ajib aliyazungumza hayo leo baada ya mchezo kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Yanga uliopigwa uwanja wa Jamhuri ambapo Mtibwa iliondoka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Riphat Khamisi kwenye dakika ya 52
Katika mchezo huo Amissi Tambwe alifunga bao kwenye dakika ya 89 hata hivyo bao hilo lilikataliwa na Mwamuzi Hans Mabena baada ya mshika kibendera kuonyesha kuwa Tambwe alikuwa ameotea
"Waamuzi hawachezeshi kwa haki kwani huwa hawako upande wetu mechi nyingi. Kwani tunajitahidi kwa uwezo wetu lakini inaumiza unapambana sana lakini anatokea mwingine anakurudisha nyuma"
Ajib amesema wataendela kupambana katika michezo iliyobaki kwani wapinzani wao Simba ambao wanawafuukuza wana mechi nyingi hivyo lolote linaweza kutokea
Baada ya mchezo huo Yanga inarejea jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa April 29 2019 kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza