Kuna la kujifunza baada ya Omog kutimuliwa Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Dec 2017
Kuna la kujifunza baada ya Omog kutimuliwa Simba
Jana uongozi wa Simba ulifikia makubaliano ya kuvunja mkataba wa aliyekuwa kocha Mkuu, Joseph Omog baada ya Simba kutolewa kwenye michuano ya kombe la FA na timu ya daraja la pili, Green Worriors.

Omog amedumu kwenye kikosi cha Simba kwa muda wa miezi 17 na ameingoza Simba kwenye michezo 79.

Ameshinda michezo 53, ametoka sare michezo 16 na kufungwa michezo 10.

Kwenye kipindi chake Simba haijawahi kufungwa na Yanga. Amekutana na Yanga mara tano, ameshinda tatu na kutoka sare mbili.

Katika msimu wake wa kwanza Omog aliiongoza Simba kutwaa taji la FA na kuwezesha kushiriki michuano ya Kimataifa msimu huu kwa mara ya kwanza baada ya miaka minne.

Aidha angeweza kutwaa ubingwa wa VPL katika msimu huo wa kwanza kama sio 'figisu' zilizofanywa na TFF.

Ni bahati mbaya tu kazi ya ukocha wakati mwingine unalazimika kuwajibishwa pale timu inapofanya vibaya lakini kwa takwimu zake Omog akiwa kikosi cha Simba, anastahili pongezi na tunamtakia kila la kheri.

Lakini uongozi wa Simba unapaswa uwe na jambo la kujifunza msimu huu hasa baada ya kutumia pesa nyingi wakati wa dirisha kubwa la usajili.

Kamati ya usajili ilijipa jukumu la kusajili wachezaji bila kumshirikisha kocha, hili Omog mwenyewe amelizungumza mara kadhaa.

Leo hii Simba ina kikosi kipana lakini bado tunaendelea kuwa na matatizo kwenye baadhi ya namba kwa nini? Tulisajili kwa pupa.

Kuna wachezaji leo hii kama Shomari Kapombe na Said Mohammed Nduda' hawajwahi kuitumikia Simba tangu wasajiliwe kwa kuwa ni majeruhi.

Tumekuwa watu wa kusajili wachezaji na kuvunja mikataba ya wengine kila siku.

Omog amewajibishwa sababu tu ni lazima awajibishwe kwa kuwa ndiye kocha Mkuu lakini kwa kiasi kikubwa baadhi ya wachezaji wamemuangusha.

Aidha wachezaji wa Kimataifa kama Okwi, Niyonzima, Gyan na Mavugo hawa wote hawakuwepo huku Mwanjali akiwa tayari ameonyeshwa mlango wa kutokea.

Simba iwe na utaratibu wa kuwabana baadhi ya wachezaji mfano Okwi ambao mara kwa mara wanaomba ruhusa kurudi kwao kushughulikia 'matatizo ya kifamilia'

Simba inahitaji kuwa na wachezaji wake muhimu katika michezo muhimu kwani lolote linaweza kutokea.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
58m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
12h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
18h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
21h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’