Samatta awashukuru mashabiki, mechi dhidi ya Burundi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
9 Sep 2019
Samatta awashukuru mashabiki, mechi dhidi ya Burundi

Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Mbwana Samatta amewashukuru mashabiki kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wa kusaka tiketi ya michuano ya kombe la dunia jana, Tanzania ikishinda kwa mikwaju ya penati 3-0

Samatta amesema sapoti ya mashabiki ilikuwa mchango mkubwa kwao kuhakikisha wanatimiza malengo ya kutinga hatua ya makundi

"Japo njia ya ushindi ilikuwa ngumu lakini mwisho tulipata tulichokitaka kama captain nikiwakilisha wachezaji wenzangu pamoja na benchi la ufundi tutakuwa wachoyo wa fadhila tusipowashukuru nyote mliojitokeza katika michezo hii miwili dhidi ya Burundi"

"Sapoti yenu ilitusukuma pale ambapo kulilega,na matokeo haya ya kufuzu hatua ya makundi ni maalum kwenu Watanzania wote mnaoisapoti timu ya taifa kwa moyo wa dhati"

"Hata wale ambao hawakupata bahati ya kufika uwanjani, na popote walipokuwa waliomba ushindi kwa moyo mmoja na pia kwa wote ambao kwa njia moja ama nyingine walitumia njia yoyote kuhamasisha wengine kuisapoti timu yao"

"Asante sana. Viva Taifa stars"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
6h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
12h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
15h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’