Mabingwa wa kihistoria Tanzania Bara Yanga leo Alhamisi wanashuka katika dimba la CCM Kirumba kuikabili Kagera Sugar kwenye mchezo wa ligi kuu
Huo utakuwa mchezo wa pili wa nyumbani kwa Yanga kupigwa katika uwanja wa CCM Kirumba msimu huu baada ya juzi kuifumua African Lyon mabao 2-0 katika uwanja huo
Yanga imekuwa na rekodi nzuri dhidi ya Kagera Sugar ikishinda michezo yote iliyopigwa misimu minne iliyopita
Mara ya mwisho kwa Yanga kupoteza mchezo dhidi ya Kagera Sugar ilikuwa Novemba 01, 2014 ambapo ilifungwa bao 1-0
Katika msimu wa 2016/17 Yanga ilipata ushindi mkubwa zaidi dhidi ya Kagera Sugar baada ya kushinda mabao 6-2 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Kaitaba
Mchezo wa leo utakuwa na ushindani wa kipekee kutokana na mazingira ya kila timu
Yanga inahitaji ushindi ili kuendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi ikiendelea kupigania ubingwa wakati Kagera Sugar yenye alama 36 inashika nafasi 17 ikiwa miongoni mwa timu ambazo ziko hatarini kuteremka daraja
Katika mchezo wa duru la kwanza uliopigwa uwanja wa Kaitaba Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1