Simba iliidharau UD Songo - Julio

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
27 Aug 2019
Simba iliidharau UD Songo - Julio

Nyota wa zamani wa klabu ya Simba Jamhuri Kiwhelo 'Julio' amesema moja ya sababu iliyopelekea Simba kuondoshwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa, ni kitendo cha kuidharau UD Songo

Julio ambaye pia amewahi kuwa kocha wa Simba, amesema baada ya matokeo ya suluhu ya bila kufungana kwenye mchezo wa ugenini, pamoja na mafanikio iliyopata Simba kwenye michuano hiyo msimu uliopita, wachezaji waliona watakuwa na kazi rahisi

"Wachezaji walijisahau, baada ya kupata suluhu ugenini kwenye mchezo wa kwanza. Lakini pia wengine wakachukulia mambo yataenda tu kama walivyofanya msimu uliopita," amesema

"Waliuanza mchezo taratibu wakati wenzao walianza kwa kasi wakihitaji kufunga bao la ugenini ambalo mwisho wa siku limewavusha"

Awaponda Wabrazil

Julio, kocha mwenye maneno mengi pia ameponda usajili wa wachezaji watatu kutoka Brazil akiwatuhumu waliofanikisha usajili huo kuwa wamehujumu fedha za Mo

"Hakuna mbrazili anayeweza kuja kucheza soka Tanzania"

"Watu wa huko wana malengo ya kucheza soka la mbele zaidi, hao wamekuja kutalii tu na si wachezaji mpira, subirini mtaona"

Awali ilielezwa kuwa wachezaji hao walisajiliwa kwa ajili ya michuano ya ligi ya mabingwa hata hivyo ni Fraga pekee aliyepata nafasi ya kucheza kwa dakika chache mchezo wa kwanza dhidi ya UD Songo

Mshambuliaji Wilker Da Silva bado ni majeruhi huku beki Tairone Santos yeye akishiriki mechi moja tu Simba Day

Hata hivyo kocha Patrick Aussems alieleza sababu ya kutowatumia wachezaji hao akisema bado wanahitaji kujifunza utamaduni wa soka la Afrika

Aidha amesema suala la lugha pia ni tatizo linalowafanya wachelewe kuzoea mazingira

Lakini alisema wameonyesha viwango vizuri, na watapewa nafasi kulingana na mahitaji ya mchezo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
11h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
14h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’