Kamusoko awaita mashabiki uwanja wa CCM Kirumba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Mar 2019
Kamusoko awaita mashabiki uwanja wa CCM Kirumba

Kiungo wa Yanga,Thaban Kamusoko amesema kuwa pamoja na ugumu wa mechi ya kesho Jumamosi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Alliance FC lakini hawana hofu juu ya ushindi na kwamba wamedhamiria kubeba Ubingwa wa michuano hiyo.

Yanga ambayo ilitua jijini hapa juzi asubuhi kwa usafiri wa Ndege ya Shirika la Air Tanzania,jioni yake walijifua kwenye uwanja wa Chuo cha Ualimu Butimba ili kujiweka sawa.

Mabingwa hao wa kihistoria,msimu huu hawakuwa na ushiriki wowote wa michuano ya kimataifa,baada ya kukosa ubingwa wa Ligi Kuu uliobebwa na Simba na ule wa Kombe la Shirikisho ulioenda kwa Mtibwa Sugar.

Kwa sasa kikosi hicho chini ya Kocha wake raia wa DR Congo,Mwinyi Zahera kinapambana vikali katika mechi zake za Ligi Kuu na FA ili kuweza kushiriki kimataifa.

Akizungumza baada ya mazoezi yao,Kamusoko alisema kuwa mchezo wao wa kesho utakuwa mgumu lakini kutoka na morari waliyonayo pamoja na dhamira yao kwenye michuano hiyo lazima washinde.

Alisema kuwa pamoja na kuwakosa baadhi ya nyota wenzao ambao kimsingi wangesaidia chochote,lakini hata waliopata bahati ya kuungana na timu watafanya vizuri.

"Tunawakabiri Alliance kwa tahadhari lakini kwa kujiamini,tuliwafunga mechi ya mwisho tuliyokutana nao kwahiyo kikubwa ni kupambana kila mmoja wetu ili kutimiza malengo”alisema Kamusoko.

Kwa upande wake Winga wa kushoto,Jafary Mohamed alisema kuwa kutokana na maandalzi waliyoyafanya lazima wafanye kweli na kwamba wanawaheshimu Alliance lakini hawawaogopi.

"Ushindi uko palepale kimsingi mashabiki wetu waje kwa wingi kutusapoti,mechi hii ni muhimu sana kwetu katika kusaka nafasi ya kusonga Nusu Fainali ya michuano hii", alisema Mohamed.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
13h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
17h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
18h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
18h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’