Nahodha msaidizi wa Simba Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' amesema wameyakubali matokeo ya kuondoshwa michuano ya ligi ya mabingwa dhidi ya UD Songo kwani ndio mpira ulivyo
Zimbwe Jr maarufu zaidi kama 'Tshabalala', amesema walifanya jitidaha kupata ushindi lakini bahati haikuwa yao
"Tulipambana ili tuweze kushinda lakini bahati haikuwa upande wetu," amesema
"hatuna namna, inabidi tujipange na michuano inayokuja mbele yetu"


Baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Gadiel Michael kwenye dakka ya 77, Tshabalala aliongeza kasi ya mashambulizi ya Simba kuelekea lango la UD Songo
Mashabiki wengi wa Simba walitaraji Tshabalala angeanzishwa upande wa kushoto hata hivyo ulikuwa uamuzi wa kocha Patrick Aussems kuanza na Gadiel
ADVERTISE HERE