Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amewaomba radhi mashabiki wa timu hiyo baada ya Simba kuondoshwa hatua ya awali michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Simba imelazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya UD Songo katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa leo
Ni matokeo yaliyoinufaisha UD Songo ikisonga mbele kwa faida ya bao la ugenini
Manara amesema matokeo haya ni msiba kwa wapenzi, wanachama na mashabiki wa klabu ya Simba
"Samahanini sana mashabiki wetu. Hakika huu ni msiba na ni fedheha kuu. Nipo tayari kuwajibika kwa matokeo haya. Nawaomba tena Samahani Washabiki wetu," Manara ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram
Uongozi wa Simba umewataka mashabiki wake kuwa watulivu na kukubali kwani ndio mpira wa miguu ulivyo, kuna wakati wa furaha na wakati wa huzuni