Sina tatizo na Manara, tutashirikiana - Macha

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Aug 2019
Sina tatizo na Manara, tutashirikiana - Macha

Afisa Habari Mpya wa klabu ya Simba Gift Macha amesema anatarajia kupata ushirikiano kutoka kwa wafanyakazi wa klabu ya Simba kama ilivyo siku zote

Macha anayetajwa kuchukua nafasi ya Haji Manara aliyepewa majukumu mapya, amesema amekuwa na ushirikiano mzuri na wafanyakazi wa Simba akiwemo Manara

"Nimekuwa nikifanya kazi vizuri na Manara, ni mtu ambaye nikiwa na shida nampigia na ataipokea simu yangu mara moja," amesema

"Naamini hakuna kitu kitabadilika baada ya mimi kuingia Simba Sc, tutaendelea kushirikiana kama kawaida"

Awali Manara alionekana hakuwa ameridhishwa na mabadiliko hayo ambayo yamepelekea yeye kuhamishwa kitengo

Lakini baada ya majadiliano na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mohammed Dewji, Manara ameonyesha kuridhia majukumu yake mapya ya uhamasishaji ambayo bado yatamfanya aendelee kuwa karibu na mashabiki wa Simba

Jana alifuta mpango wake wa kuzungumza na waandishi wa habari huku akifichua kuwa bosi Mo alimzuia

Inaelezwa jukumu kubwa la Macha ni kuboresha kitengo cha habari hasa kukiendesha kisasa

Miongoni mwa maeneo yake ni pamoja na upashaji habari kupitia kurasa za mitandao ya kijamii, kuiboresha Simba TV ambapo inaelezwa uongozi wa Simba uko mbioni kuifanya kuwa chaneli rasmi itakayopatikana kwenye ving'amuzi vyote nchini

Hivi karibuni Simba imeanzisha chaneli rasmi ya Youtube ambayo itatumika kuwapa taarifa mbalimbali mashabiki wake pale kunapotokea matukio muhimu

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
18h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’