Stars yaanza mawindo ya Uganda

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Mar 2019
Stars yaanza mawindo ya Uganda

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' jana Jumatatu kilianza mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa kusaka tiketi ya kutinga fainali za AFCON 2019, kikijiandaa kucheza na Uganda Cranes Jumapili

Stars inayoshika nafasi ya tatu kundi L ikiwa na alama tano sawa na Lesotho inayoshika nafasi ya pili kutokana na faida ya matokeo baina ya timu hizo, inahitaji kushinda Jumapili huku ikiomba Lesotho isipate ushindi katika mchezo dhidi ya Cape Verde

Stars itakuwa na kibarua cha kuifunga Uganda ambayo tayari imefuzu kwa fainali za michuano hiyo zitakazofanyika mwezi Juni nchini Misri ikiwa imejikusanyia alama 13

Katika mchezo wa kwanza baina ya timu hizo uliopigwa nchini Uganda, matokeo yalikuwa suluhu ya bila kufungana, Stars ikiwa timu pekee iliyopata pointi moja mbele ya Uganda katika kundi L

Kelvin Yondani, Feisal Salum na Gadiel Michael ni miongoni mwa wachezaji walioanza kujifua na kikosi cha Stars jana huku beki Andrew Vicent akiachwa kutokana na majeruhi nafasi yake ikichukuliwa na Erasto Nyoni

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’