Mshambuliaji wa Simba Adam Salamba ambaye ametua kwa mkopo klabu ya Namungo Fc, amesema ana matumani makubwa ya kufanya vizuri kwenye kikosi cha timu hiyo
Salamba amesajiliwa na Namungo Fc kwa mkopo wa mwaka mmoja baada ya mpango wa kutimkia Afrika Kusini kukwama
Hata hivyo Salamba amesema mpango wake wa kucheza soka Afrika Kusini ulikwama kutokana na sababu binafsi lakini huenda akarejea tena mwakani
Klabu ya TS Sporting inayoshiriki ligi daraja la kwanza ndio iliyokuwa ikimuwania
"Sikwenda kufanya majaribio TS Sporting, walinihitaji ili wanisajili moja kwa moja"
"Nimerejea nchini kutokana na sababu binafsi lakini pengine mkataba wangu ukiisha na Simba nitarudi tena," amesema
"Nimefurahi kujiunga na Namungo kwani naamini kwa kushirikiana na wachezaji waliopo, tutafanya vizuri"
Namungo imechukua nyota watatu wa Simba kwa mkopo
Pamoja na Salamba, wengine ni Paul Bukaba na Mohammed Ibrahim 'MO'